Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Vikosi dhabiti vya kulinda amani vyahitajika: Le Roy

Vikosi dhabiti vya kulinda amani vyahitajika: Le Roy

Mratibu wa masuala ya kulinda amani  kwenye Umoja wa Mataifa Alain Le Roy amesema kuwa kuna mahitaji ya kuwepo vikosi dhabiti vya kulinda amani vya Umoja wa Mataifa akiongeza kuwa hili limeshuhudiwa kwenye Jamhuri ya kidemokrasi ya Congo, nchini Ivory Coast na Sudan.

Amesema kuwa uungwaji mkono wa baraza la usalama la umoja wa Mataifa umekuwa wenye manufaa katika kuruhusu kuwepo kwa vikosi dhabiti vya wanajeshi wa Umoja wa Mataifa.

(SAUTI YA ALAIN LE ROY)

Alain  Le  Roy amekuwa mkuu wa oparesheni za kulinda amani kwenye UM kwa miaka mitatu iliyopita.