Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wanajeshi wanne wa UM wa kulinda amani eneo la Abyei wauawa

Wanajeshi wanne wa UM wa kulinda amani eneo la Abyei wauawa

Wanajeshi wanne wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Sudan wameuawa hii leo na wengine saba kujeruhiwa baada ya bomu kulipuka walipokuwa kwenye shughuli ya kupiga doria. Wanajeshi hao kutoka Ethiopia walio miongoni mwa kikosi cha umoja wa mataifa cha kulinda katika eneo la Abyei walikuwa wakipiga doria kwenye eneo la Mabok kusini mashariki mwa mji wa Abyei wakati waliuawa.

Kupitia kwa msemaji wake katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ameelezea kusikitishwa kwake kufuatia tukio hilo na pia akatoa rambi rambi zake kwa jamaa na marafiki wa wanajeshi waliouawa na kwa wale saba waliojeruhiwa. Zaidi ya wanajeshi 500 wote kutoka Ethiopia wamepelekwa kwenye eneo hilo baada ya baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kupiga kura ya kupeleka kikosi kwenye eneo la Abyei kufuatia mapigano yaliyowalazimu zaidi ya watu 100,000 kukimbia makwao.