Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mpango wa ujenzi wa endelevu wapigwa jeki

Mpango wa ujenzi wa endelevu wapigwa jeki

Mpango unaendeshwa na shirika la kimataifa wenye shabaya ya kuanzisha vigezo vya kimataifa ambavyo vitahusika na upigamaji wa wazi wa matumizi ya gezi kwenye ujenzi leo umepata msukumo mpya kufuatia shirika la kimataifa la viwango ISO kukubali kuweka vifaa vipya vitavyoupa uhai mpango huo.

ISO imesema kuwa imekubali kuangalia namna ya kuingiza vifaa vya kisasa kwa ajili ya kukaribisha ubunifu ambao utahusika moja kwa moja na upimaji viwango vya nishati inayotumiwa kwenye ujenzi.Mpango huo unaratibiwa na shirika la umoja wa mataifa linalohusika na masuala ya mazingira UNEP unajulikana kama Common Carbon Metric (CCM).Kwa kiasi kikubwa hatua hiyo imedhamiria kuleta mapinduzi kwa kukaribisha ujenzi endelevu unaozingatia mazingira.