Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wahamiaji 25 kutoka Libya wafa wakijaribu kuingia ulaya

Wahamiaji 25 kutoka Libya wafa wakijaribu kuingia ulaya

Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM linasema kuwa maiti za wahamiaji 25 zimepatika kwenye meli moja iliyokuwa ikiwasafirisha watu 300 kwenda kwa kisiwa cha Italia cha Lampedusa. IOM inasema kuwa watu 270 waliokolewa na walinzi wa pwani ya Italia.

Asilimia kubwa ya wahamiaji waliokuwa kwenye meli hiyo wametoka nchi za kusini mwa jangwa la Sahara. Pia kufuatia ghasia zinazoshuhudiwa nchini Libya IOM imewaokoa zaidi ya wahamiaji 160,000 tangu mwezi Februari. Jumbe Omari Jumbe ni msemaji wa IOM.

(SAUTI YA JUMBE OMARI JUMBE)