Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM wafanya mkutano wa dharura kuijadili Syria

UM wafanya mkutano wa dharura kuijadili Syria

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa limeita mkutano wa dharura kufuatia hatua ya serikali ya kutumia nguvu dhidi ya waandamanaji na vikosi vya serikali . Mamia ya waandamanaji wanaondamana kwa amani wanaripotiwa kuuawa.

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa amelaani ghasia akiutaka utawala nchini Syria kukoma kutumia nguvu dhidhi ya raia. Mataifa kama vile Ujerumani , Uingereza, Ufaransa ,Ureno wanataka kuwepo kwa azimio la kulaani matumzi ya nguvu yanayofanywa na serikali ya Syria dhidi ya raia. Ghasia nchini Syria zimekuwa zikiendelea tangu tangu mwezi machi mwaka huu.