Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Oparesheni ya Israel yasababisha vifo vya Wapalestina wawili

Oparesheni ya Israel yasababisha vifo vya Wapalestina wawili

Mratibu wa masuala ya amani kwenye eneo la mashariki ya kati Robert Serry ametoa wito kwa utawala nchini Israel kujizuia baada ya Wapalestina wawili kuuawa wakati wa oparesheni ya kijeshi kwenye kambi moja katika eneo la West Bank. Wanajeshi watano wa Israel nao pia walijeruhiwa kwenye oparesheni hiyo iliyoendeshwa na wanajeshi wa Isreal kwa madai ya kuweka usalama.

Akilihutubia baraza la usalama la Umoja wa Mataifa juma lililopita bwana Serry alionya kuwa mfumo wa kisiasa wa kutatua mzozo kati ya Israel na Palestina huenda ukakwamwa ambapo alitoa wito kwa pande husika kushirikiana kwa kupatikana kwa mataifa mawili. Mazungumzo ya amani kati ya Israel na Palestina yamekwama tangu mwezi Septemba baada ya Israel kukataa kuuendelea na usitishaji wa ujenzi wa makao kwenye ardhi iliyotwaliwa ya Wapalestina.