Baraza la usalama larefusha muda kwa vikosi vya UNAMID kuendelea kusalia Sudan

1 Agosti 2011

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa limerusha muda wa kuendelea kusalia vikosi vyake vya ulinzi wa amani huko Darfur vikosi ambavyo vinafanya kazi kwa nguvu ya pamoja baina ya Umoja huo wa Mataifa na Umoja wa Afrika.Vikosi hivyo UNAMID sasa vimeongezewa muda wa mwaka mmoja zaidi ili kuendelea na operesheni zake za amani katika jimbo la Darfur.

Vikikabiliwa na ufinyu wa vitendea kazi pamoja na askari, vikosi hivyo vinaandaliwa mpango wa kuviongezea vitendea kazi zaidi katika siku za usoni.Kwa mujibu wa baraza hilo la usalama, vikosi vya UNAMIDI vinapaswa kuhakikisha kwamba ustawi wa kiraia unazingatiwa vyakutosha

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter