Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ECOSOC yataka utekelezwaji wa malengo ya kielimu

ECOSOC yataka utekelezwaji wa malengo ya kielimu

Rais wa baraza la uchumi na kijamii la Umoja wa Mataifa Lazarous Kapambwe ametaka kuwepo kwa shabaya ya dhati juu ya utekelezwaji wa maazimio yaliyofikiwa na baraza hilo ambalo liliweka zingatio la uimaishwaji wa mifumo ya elimu kw amaelezo kuwa ndiyo mwarubaini wa kukabiliana na tatizo la umaskini unaoikabili dunia.

Rais huyo wa ECOSOC amesema kuwa ni vyema masuala mtambuko yaliyoko kwenye elimu yakatekelezwa ipasavyo ili kuyapiga jeki makundi maalumu ikiwemo watoto wa kike ambao wanakabiliwa na kikwazo cha kufikiwa ipasavyo na elimu.Amesisitiza kuwa ili dunia ifikie shabaya ya kuukabili umaskini kwanza inawajibika kuvunja kongwa la kitabaka ambalo linayaacha nyuma baadhi ya makundi ya watu kufikiwa na elimu.