Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Makabiliano yashuhudiwa kati ya vikosi vya Lebanon na Israel

Makabiliano yashuhudiwa kati ya vikosi vya Lebanon na Israel

Umoja wa Mataifa unasema kuwa umeanzisha uchunguzi kufuatia ufyatulianaji wa risasi uliotokea mapema leo kati ya wanajeshi wa Lebanon na Israel kwenye mpaka kati ya nchi hizo mbili.

(SAUTI YA MAUREEN KOECH)

Kulingana na kikosi cha kulinda amani nchini Lebanon UNIFIL, ufyatulianaji huo ulitokea katika eneo lijulikanalo kama Blue Line linalotenganisha hizo hizo mbili. Kamanda wa kikosi cha UNIFIL Jenerali Santi Bonfanti anawasiliana na makamanda wa pande zote mbili akiwashauri kusitisha makabiliano hayo. Kuliheshimu eneo la Blue Line ni azimio la baraza la usalama la Umoja wa Mataifa lililomaliza mzozo ulioibuka mwaka 2006 kati ya Israel na kundi la Hezbollah nchini Lebanon.