Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban alaani mauaji yanayoendeshwa na wanajeshi wa serikali nchini Syria

Ban alaani mauaji yanayoendeshwa na wanajeshi wa serikali nchini Syria

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa ameelezea kushangazwa kwake na ripoti kutoka nchini Syria kuwa mamia ya waandamanaji wameuawa kwenye mji wa Hama na miji mingine kote nchini Syria. Ban amelaani vikali matumizi ya nguvu dhidi ya raia na kutoa wito kwa serikali ya Syria kusitisha ghasia hizo mara moja.

Ban amesema kuwa serikali ya Syria ina wajibu wa kuheshimu haki za binadamu za watu wake ikiwemo haki ya kusema na haki ya kukusanyika kwa amani. Kupitia kwa msemaji wake Ban pia anaikumbusha serikali ya Syria kuwa itawajibika chini ya sheria za kimataifa kwa vitendo vyote ambayo imeendesha dhidhi ya raia. Kulingana na ripoti za vyombo vya habari wanajeshi wa Syria wamewaua watu kadha kwenye mji wa Hama.