Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM walaani ghasia za kuipinga serikali zinazoshuhudiwa nchini Malawi

UM walaani ghasia za kuipinga serikali zinazoshuhudiwa nchini Malawi

Mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Ravina Shamdasani ametaka kusitishwa kwa ghasia nchini Malawi kufuatia ripoti za kuuawa kwa waandamanaji kadha na wanajeshi wa serikali juma lililopita.

Waandamaji hao wamekuwa wakiitisha kuwepo kwa uhuru na haki za binadamu huku pia wakilalamikia uhaba wa mafuta na fedha za kigeni. Shamdasani anasema kuwa kuna haja ya kufanyika kwa uchunguzi kufuatia kuwepo madai ya ukiukaji wa haki za binadamu.

(SAUTI YA RAVINA SHAMDASANI)