Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Jitihada za AMISOM kulinda amani nchini Somalia

Jitihada za AMISOM kulinda amani nchini Somalia

Makala yetu wiki hii inaangazia jitihada za kikosi cha kulinda amani cha muungano wa Afrika nchini Somali cha AMISOM katika kuweka usalama na kukabiliana na makundi yaliyo na nia ya kuiangusha serikali ya mpito ya Somalia na pia katika kuhakikisha kuwa misaada imewafikia mamilioni ya watu ambao kwa sasa wanakabiliwa na njaa.

Somali ni nchi ya pembe ya Afrika ambayo haijakuwa na serikali dhabiti kwa zaidi ya miaka ishirini iliyopita.Nchi ya Somali imeshuhidia mapigano ya muda mrefu kati ya makundi hasimu ya wanamgambo na pia kati ya serikali ya mpito na wanamgambo.

Kwa sasa kikosi cha kulinda amani cha Muungano wa Afrika nchini Somalia AMISOM kilicho na zaidi ya wanajeshi 9000 kiko nchini Somalia kwa minajili ya kuweka amani kwenye taifa ambalo kwa sasa pia linakumbwa na hali mbaya ya ukame na njaa.Kikosi hicho ambacho asilimia kubwa ya wanajeshi wake wanatoka nchini Uganda kina wajibu mkubwa wa kuhakikisha kuwa makundi ya wanamgambo hasa kundi la Al Shabaan hayaingushi serikali ya mpito.

Lakini pia kwa sasa vikosi kikosi hicho kimejipata kwenye wajibu wa kuhakikisha kuwa mashirika ya Umoja wa Mataifa ya kutoa misaada nchini Somalia na mengineyo yana usalama wa kutosha yanaposambaza misaada kwa maelfu ya watu walio kwenye hatari ya kufa njaa.Kamanada wa kikosi cha AMISOM anayeondoka meja Jenerali Nathan Mugisha anasema kuwa wamefanikiwa pakubwa katika kuhakikisha kuwa misaada imewafikia walioathiriwa na njaa kwa kuhakikisha kuwa wamepata usalama wa kutosha pia wamefaniwa katika kuyazuia makundi ya wanamgambo yaliyo na nia ya kuiangusha serikali ya mpito.

(MAHOJIANO NA NATHAN MUGISHA)