Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM wahaidi kuendelea kuisadia Pakistan

UM wahaidi kuendelea kuisadia Pakistan

Umoja wa Mataifa umehaidi leo kuwa utaendelea kuipiga jeki Pakistan katika wakati ambapo nchi hiyo inaendelea kujitutumua kujijenga upya baada ya mafuriko ya mwaka uliopita yaliyosababisha hasara kubwa.Mafuriko hayo ambayo ni tukio kubwa kuwahi kuikumba nchi hiyo, yalisambabisha zaidi ya watu milioni 20 kuathiriwa.

Watu zaidi ya 2,000 walipoteza maisha na nyumba zipatazo milioni 1.6 zikiharibiwa.Kulingana na mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa kwenye eneo hilo Rauf Engin Soysal,ametilia uzito juu ya kuendelea kupigwa jeki kwa nchi hiyo.Amesema kuwa Umoja wa Mataifa utaendelea kunyosha mkono kwa wananchi wa taifa hilo na serikali yao ili hatimaye kufanikisha harakati za kulijenga upya taifa hilo.