Kuna haja ya kuwa na mchakato wa ufikiaji suluhu Libya-UM

29 Julai 2011

Umoja wa Mataifa umeainisha hatua zinazoweza kuzika mzozo wa Libya kwa kusema kuwa lazima kuanzishwa mchakato wa maridhiano ili kukaribisha kipindi cha mpito kuelekea kwenye maamuzi ya umalizwaji wa mzozo huo.Kwa mujibu wa mtaalamu wa masuala ya kisiasa ndani ya Umoja huo wa Mataifa, Libya inapaswa kufukia makubaliano ya kusitisha mapigano.

Akizungumza kwenye kikao cha Baraza la Usalama Lynn Pascoe amesema kuna haja sasa ya pande zinazozozana kuketi pamoja ili kukaribisha makubaliano ya utanzuaji wa mzozo huo.Ameelezea pia juhudi zinazoendelea kuchukuliwa na wanadiplomasia wa Umoja wa Mataifa wanaofanya mazungumzo na pande zote mbili wakijaribu kuleta sura ya ufikiwaji muafaka wa maridhiano.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud