Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban kumchagua mwanadiplomasi wa Uholansi kumwakilisha Afrika Magharibi

Ban kumchagua mwanadiplomasi wa Uholansi kumwakilisha Afrika Magharibi

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ametangaza kusudio lake la kutaka kumteua mwanadiplomasia wa Uholansi kuwa mwakilishi wake nchini Ivory Cost na kusimamia vikosi vya kulinda amani katika eneo la afrika magharibi. Ban amesema kuwa anatazamiwa kumteua Bert Koenders ili kuchukua nafasi ya Choi Young-jin ambaye muda wake unatazamiwa kumalizika August 31 mwaka huu.

Akielezea utendaji kazi wa mwanadiplomasia huyo anayemaliza muda wake ambaye ni raia wa Korea, Ban ameusifu utumishi wake akisema kuwa aliwajibika kwenye utendaji bira wa kazi.Mwanadiplomasia huyo mpya anaelezwa kuwa ni mtu mwenye uwezo mkubwa na anatazamiwa kuleta uzoefu wake wa zaidi ya miaka 25 kwenye masuala ya kimataifa kwenye eneo hilo la afrika magharibi.