UNESCO yalaani mauaji ya waandishi wa habari nchini Mexico na Brazil

29 Julai 2011

Shirika la Umoja wa Mataifa linalotetea uhuru wa wanahabari hii leo limelaani vikali mauaji ya waandishi wa habari nchini Mexico na Brazil mataifa ambayo pia waandishi wa habari kadha wameuawa mwaka huu. Mkurugenzi mkuu wa shirika la elimu , sayansi na utamaduni la moja wa Mataifa (UNESCO) Irina Bokova ametaka waliohusika kwenye mauaji ya Yolanda Ordaz de la Cruz nchini Mexico na Auro Ida nchini Brazil kufikishwa mbele ya sheria na kutoa wito kwa hatua zaidi kuchukuliwa ili kuuzia mashambuilizi dhidi ya waaandishi wa habari.Bi Ordaz de la Cruiz ni mwandishi wa habari wa tatu kutoka gazeti la Notiver kuuawa mwaka huu.

Kulingana na shirika moja lisilokuwa la kiserikali waandishi watano wameuawa nchini Mexico mwaka huu, huku wanne kati yao wakiuawa kwenye jimbo la Veracruz. Ida mwenye umri wa miaka 53 na ambaye alikuwa akichunguza ufisadi alipigwa risasi na mtu asiyejulikana akiwa ndani ya gari lake.

 

Shiriki kwenye Dodoso UN News 2021:  Bofya hapa Utatumia dakika 4 tu kukamilisha dodoso hili.

♦ Na iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter