Mapigano mjini Mogadishu yahatarisha maisha ya raia

29 Julai 2011

Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR linasema kuwa mapigano mapya yanayoendelea kati ya vikosi vya serikali na kundi la wanamgambo la Al Shabab kwenye mji mkuu Mogadishu yameyaweka maisha ya raia kwenye hatari.

Fatoumata Lejeune-Kaba kutoka UNHCR anasema kuwa mapigano hayo yamehatarisha maisha ya raia na zaidi ya watu 100,000 waliokimbia njaa kutoka maeno ya kusini mwa Somalia.

(SAUTI YA FATOUMATA LEJEUNE-KABA)

Kwa sasa idadi kubwa ya wasomali wanaendelea kuingia nchini Kenya na Ethiopia wakikimbia mizozo na njaa.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter