Mamia ya Wasomali wanaokimbia njaa watembea kwenda Kenya

29 Julai 2011

Kenya imeufunga mpaka kati yake na Somalia wakati ambapo watu wanapojaribu kukimibia njaa kusini na kati kati mwa Somalia kwa miguu. Kambi ya Daadab ambayo kwa sasa ni makao ya wakimbizi 360,000 inawapokea wakimbizi zaidi.

Msemaji wa IOM Jumbe Omari Jumbe anasema kuwa mamia ya wasomali waliochoka wako kwenye barabara ya kutoka mji ulio kwenye mpaka wa Liboi kwenda kambi ya Daadab

(SAUTI YA JUMBE)

Hata hivyo Jumbe anasema kuwa IOM itatoa usafiri kwa wasomali walio barabarani kwenye kambi ya Daadab nchini Kenya.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter