Zaidi ya watoto milioni moja wahitaji misaada ya dharura kusini mwa Somalia

29 Julai 2011

Huku takriban watoto milioni 1.5 kote nchini Somalia wakiwa wanahitaji misaada ya kuokoa maisha na wengine 640,000 wakisumbuliwa na utapiamlo shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF limetoa wito kwa washika dau wote kulipa kipau mbele suala la kuokoa maisha na kufanya jitihada za kuwafikia watoto wanaohitaji usaidizi.

Ili kuwafkia watoto hao kwa haraka UNICEF pamoja na washirika wake wameanzisha mikakati ya kuhakikisha kuwa misaada imefika kwenye maeneo waliko. Marixie Marcado ni msemaji wa UNICEF.

(SAUTI  MARIXIE MARCADO)

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter