UM waongeza muda wa kuhudumu wa kikosi chake nchini Iraq

28 Julai 2011

Baraza la usalama la Umoja wa Matifa limeongeza muda wa kuhudumu wa kikosi chake cha kulinda amani nchini Iraq (UNAMI) wakati pia ikikaribisha mafanikio ya kuimarika kwa usalama yaliyopatikana lakini haya hivyo UM umesisitiza hatua zaidi kupigwa katika masuala ya kibinadamu, haki za kibidamu na siasa.

Kulingana azimio lililopitishwa ni kuwa usalama umeimarika nchini Iraq na hatua zaidi zinaweza kupigwa kupitia kwa majadiliano ya kisiasa. Wanachama wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa waaliishauri serikali kuwa kwenye mstari wa mbele katika kupigania haki za binadamu kwa kuunga mkono tume huru ya haki za binadamu nchini humo na kuweka mikakati ya kuhakikisha kuwa wanawake wanaweza kutekeleza wajibu mkubwa kwenye jamii.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter