Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mafunzo ya mtandaoni yaanzishwa ili kuimalisha hali ya usalama wa chakula

Mafunzo ya mtandaoni yaanzishwa ili kuimalisha hali ya usalama wa chakula

Katika juhudi za kukabiliana na mkwamo wa ukosefu wa chakula, kamati ya usalama wa chakula duniani imeanzisha jukwaa maalumu ambalo litawajibika na utowaji ushari kupitia mtandao wa mawasiliano.Taarifa iliyotolewa na kamati hiyo imesema kuwa kusudio kubwa la kuanzishwa kwa ushauri wa mtandaoni inalenga kusaidia maeneo ambayo yanakwama juu ya usalama wa chakula.

Njia itakayotumika kufanikisha utendaji kazi wake ni pamoja na kukaribisha majadiliano ya wazi yakiwahusisha wananchi wa kada mbalimbali.Kitengo hicho kitakuwa wazi hadi October 15 mwaka huu na matokeo ya majadiliano hayo yanatazamiwa kuwasilisha kwenye mkutano wa kamati hiyo utakaofanyika baadaye Rome, Italy.