Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Upatikanaji wa maji safi na salama ni haki ya msingi-Afisa wa UM

Upatikanaji wa maji safi na salama ni haki ya msingi-Afisa wa UM

Afisa wa Umoja wa Mataifa amesisitiza haja ya kuimarishwa kwa mifumo ambayo itahakikisha kunafikiwa usawa kwenye upatikanaji wa maji safi na salama akisema kuwa hatua hiyo ndiyo muhimu hasa wakati huu kunakopiganiwa shabaya ya kukabuliana na umaskini.Rais wa baraza kuu la Umoja wa Mataifa amesema kufikiwa shabaya ya malengo ya mellenia hasa lengo la kukabiliana na umaskini ni agenda inayopaswa kupiganiwa kwa kuzingatia pia maeneo mengine kama vile uimarishwaji kwa afya za watoto na kudhibiti magonjwa.

Mwaka uliopita wa 2010 mkutano mkuu wa Umoja wa Mataifa ulipitisha azimio lilidai kuwa upatikanaji wa maji safi na salama ni vipaumbele vinavyopaswa kutumbukizwa kwenye haki za binadamu.Inakadiriwa kuwa zaidi ya watu milioni 900 duniani kote hawafikiwa na huduma za maji safi na salama.Kulingana na Joseph Deiss dunia inapaswa kuzingatia haja ya kutoa matumaini ya kupatikana kwa maji safi na salama kwani kiwango hicho ni kukubwa mno kwa ustawi wa maendeleo.