Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ni miaka sitini ya mkataba wa kulinda wakimbizi wa UM

Ni miaka sitini ya mkataba wa kulinda wakimbizi wa UM

Imetimia miaka 60 tangu kutekelezwa kwa mkataba la Umoja wa Mataifa lililokuwa na lengo la kutatua tatizo la wakimbizi barani Ulaya baada ya vita vikuu vya pili vya dunia. Mkataba hu kuhusu hali ya wakimbizi ulieleza wazi nani anayestahili kuitwa mkimbizi na ni haki gani zilizo kati ya nchi waliko wakimbizi na wakimbizi wenyewe.

Mkataba huo umeliwezesha shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR kusaidia mamilioni ya watu waliohama makwao kwa muda wa miongo sita iliyopita . Vivian Tan msemaji wa UNHCR kutoka Geneva na alizungumzia zaidi azimio hilo.

(SAUTI YA VIVIAN TAN)