Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ufadhili wa misaada kwenda pembe ya Afrika waendelea kutolewa

Ufadhili wa misaada kwenda pembe ya Afrika waendelea kutolewa

Ufadhili zaidi unaendelea kutolewa kwa muda wa siku chache zilizopita kusaidia katika usambazaji wa misaada kwenye pembe ya Afrika. Shirika la mpango wa chakula duniani WFP linasema kuwa limepokea ahadi za zaidi ya dola milioni 250 kutoka kwa serikali , makampuni , na watu binafsi kusaidia kuwalisha watu walio kwenye hatari ya kufa njaa.

Awali WFP iliendesha oparesheni yake ya kwanza ya kusafirisha chakula kwa ndege kwenda mji mkuu wa Somalia Mogadishu ambapo maelfu ya watu wanasumbuliwa na njaa hasa watoto. Tani 10 za chakula zilisafirishwa huku tani zingine 80 zikitarajiwa kusafirishwa katika majuma machache yajayo. Hii ni moja ya oparesheni za WFP za kusaidia watu milioni 12 wanaohitaji chakulakwa dharura kwenye pembe ya Afrika.