Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM walaani shambulizi kwenye kituo cha watoto kwenye ukanda wa Gaza

UM walaani shambulizi kwenye kituo cha watoto kwenye ukanda wa Gaza

Umoja wa Mataifa umelaani shambulizi lililofanyika kwenye kituo chake cha mashindano ya msimu wa joto kwenye ukanda wa Gaza na kuapa kuwa jaribio la maelfu ya watoto wa kipalestina la kutaka kuweka rekodi mpya ya dunia kwa kurusha tiara litaendelea jinsi lilivyopangwa.

Kulingana na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbiziwa wa kipalestina UNRWA, watu 10 walikivamia na kukiharibu kituo hicho kilicho kaskazini magharibi mwa Gaza. Wavamizi hao walichoma bendera ya Umoja wa Mataifa na kuchoma sehemu moja ya jukwaa.

(SAUTI YA ALICE KARIUKI)