Ban asema kuna njia ya kuendela na shughuli ya kupunguza zana hatari duniani

27 Julai 2011

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema kuwa makubaliano ya kupunguza silaha duniani yamekwama na kupendekeza njia za kuondoa kizingiti kilichopo ikiwemo kuwateua watu mashuhuri , kubuni kamati ya dharura ya baraza kuu la Umoja wa Mataifa.

Mkutano wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa mjini New York ulikubaliana na masula ya mkutano wa 23 wa Umoja wa Mataifa wa kupunguza silahali uliofanyika mjini Matsumoto nchini Japan ambapo mkuuu wa shirika la nishati ya nuklia duniani IAEA Yukiya Amano alisitiza kuwa mataifa yote ni lazima yaheshimu mkataba wa kimataifa wa kupuunguza zana za kinyuklia. Amano amesema kuwa tangu achukue uongozi wa shirika hilo mwezi Disemba mwaka uliopa lengo lake limekuwa ni kulinda makubaliano kati ya wanachama wa mkataba na shirika la IAEA na kuhakikisha kuwa kila azimio la Umoja wa Mataifa limetekelezwa kikamilifu.

 

♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter