Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM katika jitihada za kuangamiza homa ya manjano

UM katika jitihada za kuangamiza homa ya manjano

Umoja wa Mataifa hapo kesho utaadhimisha siku ya homa ya manjano duniani kwa mara ya kwanza kabisa kama hamasisho la ugonjwa huo unaoathiri mmoja kati ya watu watatu duniani . Mkurugenzi mkuu wa shirika la afya duniani WHO Margaret Chan anasema kuwa inaeleweka kinachohitajika kufanyika akiongeza kuwa homa ya manjano ni moja ya magojwa hatari zaidi duniani.

Muungano wa homa ya manjano duniani ambalo ni shirika lisilokuwa la kiserikali umekuwa ukitumia tarehe 28 mwezi Julai kama tarehe ya kutoa hamasisho kuhusu ugonjwa huo. Kauli mbiu ya kampeni hiyo “ujue , ukabili , homa ya manjano inamuathiri yeyote, popote” ilibuniwa kueleza ukweli kuwa zaidi ya watu bilioni mbili wamaeathiriwa na ugonjwa huu na kila mwaka vifo milioni moja husababishwa na ugonjwa huu.