Ni makosa makubwa kufungamanisha mashambulizi ya Norway na Uislam Mtaalam wa UM

27 Julai 2011

Mtaalamu wa Umoja wa Mataifa anayehusika na maeneo ya uhuru wa kuabudu amesema kuwa taarifa za awali za vyombo vya habari ambazo zilihusisha tukio la mauwaji ya kutisha ya huko Norway na magaidi wa kiislamu kuwa ni taarifa zakuuzi na kufedhehesha zilizokimbilia kuaminisha mambo yasiyo ya kweli.

Mtaalamu huyo Heiner Bielefeldt amesema hali iliyojitokeza nchini humo ambako baadhi ya makundi ya watu kujaribu kuhusisha tukio hilo la mauwaji na waslamu wenye msimamo mkali,siyo tu kwamba inakera lakini pia inajenga picha ya kutaka kuaminisha tukio lisilokuwepo.

Ametaka makundi hayo kuweka kando misingi ya kukimbilia kutoa hitimisho la mambo pasipo kwanza kusubiri ukweli wenyewe .Katika tukio hilo la kutisha lililotokea jumapili iliyopita, zaidi ya watu 75 walipoteza maisha na wengine kadhaa wakijeruhiwa.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter