Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM watumia sanaa Sudan kukuza amani

UM watumia sanaa Sudan kukuza amani

Ikijitwika jukumu la kusukuma mbele ustawi wa amani,usalama na maridhiano vikosi vya muungano wa pamoja wa Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika vilivyoko Darfur nchini Sudan UNAMID vimetumia njia ya sanaa kama sehemu ya kuhamasisha wananchi kuiunga mkono hatua inayoendeshwa ya kuachana na silaha na kurejea kwenye mafungamano ya kawaida.

Tukio hilo la sanaa ya jukwani ambalo limefanyika katika eneo la El Srief lililoko umbali wa kilometa 45 kutoka kaskazini mwa Darfur limefanyika kwa shabaya ya kukuza uwelewa wa utekelezwaji wa mpango unaofahamika DDR ambao unahimiza kuweka chini silaha, kurejea kwenye jamii ya kawaida na mafungamano mapya.Ili kuleta ujembe hai kwa wananchi, nyimbo kadhaa ziliimbwa pamoja na matukio ya uchezaji ngoma na michezo mingine ya kawaida.Mpango huo umefadhiliwa na shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na maendeleo UNDP.