Belarus yakiuka sheria na kuwanyonga wafungwa kwa mara ya pili

27 Julai 2011

Kamati ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa imesema kuwa Belarus imekiuka sheria kwa kuwanyonga wafungwa wawili ambao kesi zao zilikuwa zikichunguzwa na kamati hiyo na hata baada ya ombi kwa serikali la kuitaka isubiri matokeo ya kamati hiyo. Wawili hao walikuwa wamedai kuwa waliteswa wakati wa uchunguzi na hawakupewa hukumu ya haki.

Kamati hiyo iliiomba Belarus kutowanyoka wawili hao kwa kuwa kesi zao zilikuwa zikichunguzwa . Tarehe ya kunyongwa kwa wawili hao hadi sasa haijulikani lakini huenda wamenyongwa kati ya 13 na 19 mwezi huu. Hii ndiyo mara ya pili wafungwa ambao kesi zao zinachunguzwa na kamati ya haki za binadamu ya Umoja wa Matifa wamenyongwa nchini Belarus. Mwezi machi mwaka uliopita wafungwa wengine wawili walinyongwa hata baada ya kamati hiyo kutuma ombi la kusimamishwa kunyongwa kwao kwa muda.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter