Ni mwaka mmoja tangu kutokea kwa mafuriko nchini Pakistan

27 Julai 2011

Ni mwaka mmoja sasa tangu kutokea kwa mafuriko nchini Pakistan mafuriko ambayo yametajwa kuwa janga baya zaidi la kiasili katika nyakati hizi. Mafuriko hayo yaliathiri eneo kubwa la nchi ambapo watu 2000 waliuawa na kuwaathiri wengine milioni 20 na nyumba milioni 1.6 kuharibiwa.

Uharibifu kwenye sekta ya kilimo ambayo ni tegemeo la asilimia 80 ya watu walioathirika ilikadiriwa kuwa hasara ya dola bilioni 5 . Kati ya maeneo yaliyoathirika ni pamoja na mkoa wa Punjab na sehemu kubwa ya maeneo yaliyo na rutupa nzuri nchini Pakistan.

(SATI YA ALICE KARIUKI)

Mashirika ya kutoa misaada ya kibindamu yalifanya hima kuokoa hali baada ya chakula na mali nyingine kusombwa na mafuriko. Mwaka mmoja baadaye jitahada hizo zinaonekana kuzaa matunda . Zaidi ya mshirika 20 yaliungana chini ya uongozi wa shirika la kilimo na mazao la Umoja wa Mataifa FAO ili kukabilina na changamoto zilizokuwepo yakisadiwa na wafadhili na hadi sasa zaidi ya watu milioni 7 wamerejea kwenye maisha ya kawaida.

Hata hivyo bado jitihada zaidi zinahitajika ili kuboresha maisha ya wanaoishi vijijini na kuongeza chakula. FAO inasema kuwa hadi sasa inahitaji dola milioni 96 kusaidia watu 430, 000 kwenye wilaya zilizoathirika zaidi na mafuriko kwa muda wa  miaka miwili ijayo.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter