Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watetezi wa haki za binadamu bado wanakabiliwa na hatari maishani

Watetezi wa haki za binadamu bado wanakabiliwa na hatari maishani

Mjumbe maalum kwenye Umoja wa Mataifa Margaret Sekaggya amesema kuwa si jambo rahisi kuwa mtetezi wa haki za binadam akiongeza kuwa kwenye nchi zingine ni suala hatari zaidi. Sekaggya ameyasema haya wakati wa uzinduzi wa mwongozo wake kuhusu haki ya kutetea haki za binadamu, mwongozo ulio na lengo la kuunga mkono wale wanaotetea haki za binadamu na kutoa hamasisho kuhusu hatari zinazowakabili.

Amesema kuwa watetezi wa haki za binadamu wanaendelea kudhulumiwa akiongeza kuwa anaamini kuwa mwongozo huo utachangia katika kuwepo kwa mazingira salama kwa wanaotetea haki za binadamu ili waweze kufanya kazi yao.