Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Umoja wa Mataifa walaani shambulizi dhidi ya vikiosi vyake nchini Lebanon

Umoja wa Mataifa walaani shambulizi dhidi ya vikiosi vyake nchini Lebanon

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban ki-moon pamoja na Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa wamelaani vikali shambulizi lililotekelezwa dhidi ya msafara wa magari uliokuwa ukisafirisha vikosi vya kulinda amani vya Umoja wa mataifa kusini mwa Lebanon ambapo wanajeshi watano walijeruhiwa.

Kulingana na msemaji wake Ban amesikitishwa na shambulizi hilo lililofanyika katika eneo la Saida lili kilomita 55 kutoka kwa kituo cha wanajeshi cha Nagoura.

(SAUTI YA GEORGE  NJOGOPA)