Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mamilioni ya watoto wapata chanjo ya ugonjwa wa surua nchini DRC

Mamilioni ya watoto wapata chanjo ya ugonjwa wa surua nchini DRC

Karibu watoto milioni 3.1 kwenye Jamahuri ya Kidemokrasia ya Congo wamechanjwa dhidi ya ugonjwa wa surua kwenye kampeni inayoongozwa na Umoja wa Mataifa ili kukabiliana na mkurupuko wa ugonjwa ambao umewaua zaidi ya watoto 1000 tangu mwanzo wa mwaka huu.

Shirika la kuratibu masuala ya kibinadamu OCHA linasema kuwa ugonjwa huo umewaathiri jumla ya watoto 115,600 kati ya mwezi Januari na Juni. Kampeni hiyo iliyong’oa nanga tarehe 10 mwezi Mei iliongozwa na shirika la afya duniani WHO kwenye mikoa ya Katanga, Kasai Occidental, Bas-Congo, Equateur na Orientale. Visa 5,400 vya ugonjwa wa surua viliripotiwa nchini DRC mwaka uliopita ambapo watoto 82 waliaga dunia ikilinganishwa na visa 899 na vifo 29 vilivyoripotiwa mwaka 2009.