Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM waonya kuvunjika kwa mazungumzo ya kutafuta amani kati ya Israel na Palestina

UM waonya kuvunjika kwa mazungumzo ya kutafuta amani kati ya Israel na Palestina

Mjumbe wa ngazi ya juu wa Umoja wa Mataifa anayehusika na mpango wa amani katika eneo la Mashariki ya kati Robert Serry ameonya kuwa mpango wa kutatua mzozo kati ya Israel na Paletina huenda ukasambaratika. Akihutubia mkutano wa Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa Serry amesema kuwa pande zote zinastahili kushirikiana kwa lengo lakupatikana kwa mataifa mawili na akaitaka jamii ya kimataifa kusaidia pande hizo mbili kuendelea na mazungumzo.

Mazungumzo ya amani kati ya Israel na Palestina yamekwama tangu mwezi Septemba mwaka uliopita baada ya Israel kukataa kuongeza muda wa usitishaji wa ujenzi wa makaazi kwenye ardhi iliyotwaliwa ya Wapalestina.