Baraza la Usalama lalaani kuendelea kutumiwa watoto kwenye mizozo huko CAR

26 Julai 2011

Baraza la usalama limelaani vikali mwenendo unaoendelea kuchukuliwa na makundi korofi huko Jamhuri ya Kati ambayo huwatumia watoto kama askari kwenye mizozo ya vita na kuyataka makundi hayo kuachana na mwenendo huo. Katika taarifa yake baraza hilo la usalama limeyataka makundi hayo kuwajibika kutekeleza mkataba wa makubaliano uliosainiwa hivi karibuni ambao ulipiga marafuku utumikishaji watoto kwenye mizozo ya vita.

Mkataba huo uliyataka makundi yote yanayoendelea kuwatumia watoto hao kuanza kuwaondosha mara moja.Aidha Baraza hilo la usalama limeelezea masikitiko yake kutokana na kukosekana kwa huduma za usamaria mwema kwenye maeneo yanayoshikiliwa na makundi korofi ikiwemo lile linalohodhiwa na kundi la (CPJP) lililoko kaskazini mashariki wan chi hiyo.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter