Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Idadi ya wanaokimbilia Mogadishu yazidi kuongezeka

Idadi ya wanaokimbilia Mogadishu yazidi kuongezeka

Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa linasema kuwa karibu watu 100,000 waliohama makwao wamewasili kwenye mji mkuu wa Somalia Mogadishu kwa mda wa miezi miwili iliyopita wakitafuta makao, maji na chakula baada ya kukimbia maeneo yanayokumbwa na njaa.

Umoja wa Mataifa na mashirika mengine ya kutoa misaada kwa sasa yanahitaji karibu dola bilioni 1.6 kuwasiadia mamilioni ya watu walioathiriwa na ukame nchini Somalia na meneo mengine ya pembe ya Afrika . Vivian Tan ni msemaji wa UNHCR mjini Geneva na anasema kuwa kwa sababu ya kuongezeka kwa idadi ya watu wanaohama makwao kutafuta chakula misaada inayosambazwa haitoshi, hali ambayo imesababisha kutokea kwa makabilino na uporaji.