Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNHCR na wasiwasi wa kurejeshwa nyumbani watafuta hifadhi raia wa Eritrea kutoka Sudan

UNHCR na wasiwasi wa kurejeshwa nyumbani watafuta hifadhi raia wa Eritrea kutoka Sudan

Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR limelaani kurejeshwa nyumbani kwa watafuta hifadhi kutoka Eritrea walioingia nchini Sudan ambapo mtafuta hifadhi mmoja alikufa na mwingine kujeruhiwa vibaya. Kisa hicho kilitokea mashariki mwa Sudan wakati wa shughuli ya kuwarejesha makwao watafuta hafadhi ambapo wawili kati yao waliruka kutoka kwa lori lililokuwa likiwasafirisha kwenda kwa mapaka kati ya Sudan na Eritrea.

UNHCR ina wasiwasi kuhusu kuongezeka kurejeshwa nyumbani kwa watafuta hifadhi raia wa Eritrea wanaoingia Sudan . Tangu mwezi mei mwaka huu Sudan imewarejesha nyumbani karibu watafuta hifadhi 30 pamoja na wakimbizi kwenda Eritrea ambapo UNHCR inaamini kuwa huenda wakakabiliwa na sheria.