Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mauzo ya nje yazikuamua nchi za Asia na Pacific kutoka kwenye hali mbaya ya uchumi: UM

Mauzo ya nje yazikuamua nchi za Asia na Pacific kutoka kwenye hali mbaya ya uchumi: UM

Tume ya Umoja wa Mataifa inayohusika na masuala ya uchumi na kijamii kwa nchi za Asia na Pacific (ESCAP) imesema kuwa mauzo ya nje yamezikwamua nchi kutoka kwenye hali mbaya ya uchumi duniani lakini ikaongeza kuwa itakuwa vigumu kuwepo kwa ukuaji zaidi iwapo hakutakuwa na masoko mapya katika maeneo hayo.

Nchi zilizostawi bado zinasalia kuwa masoko yanayoongoza kwa bidhaa kutoka kwa mataifa ya Asia na Pacific. Ripoti hiyo pia inaonyesha kuwa nchi za Asia na Pacific zinaongoza kwa mauzo ya nje kwa bidhaa nyingi na hata teknolojia.