Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

OCHA yatoa fedha kukabili janga la njaa katika Pembe ya Afrika

OCHA yatoa fedha kukabili janga la njaa katika Pembe ya Afrika

Kitengo cha Umoja wa Mataifa kinachohusika na usimamizi wa misaada ya kibinadamu kimetoa kiasi cha dola za kimarekani milioni 51 kwa ajili ya kusaidia shughuli za upelekaji wa misaada ya chakula katika maeneo ya Pembe ya Afrika ambayo yanakabiliwa na janga la njaa.Kumekuwa na janga la njaa linalowaandama maelfu ya watu walioko katika maeneo ya Kusini mwa Somalia .

Kitengo hicho kinachoratibu matukio ya dharura hata hivyo kimechanganua mafunga hayo ya fedha ambayo pia yatanufaisha maeneo mengine kama Ethiopia na Kenya.Kulingana na shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na misaada ya kiutu OCHA, kiasi hicho cha fedha kilitolewa wiki chache zilizopita kwa ajili ya kufadhilia shughuli mbalimbali za dharura.