Askari wa UNAMID huko Darfur washambuliwa

25 Julai 2011

Walinzi wa amani waliochini ya mwavuli wa muunganiko wa vikosi vya Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika UNAMID wanoendesha operesheni ya amani huko Darfur wamejuruhiwa baada ya kushambuliwa na watu wenye silaha katika eneo lenye mzozo la magharibi wa Sudan.

Walinzi hao wawili wakiwa katika hali ya kawaida, walivamiwa na watu wenye silaha wasiojulikana na kuwafyatulia risasa zilizowasababishia majera katika sehemu kadhaa.Mmoja anaarifiwa kuwa katika hali mbaya na amelazwa katika hospitali moja mjini Khartoum kutokana na majeraha makubwa aliyoyapata kwenye sehemu za bega.Mashambulizi hayo yalijiri wakati vikosi vya askari hao wakisindikiza msafara wa magari ya mafuta yaliyokuwa yakielekea kwenye makambi.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter