Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Australia na Malaysia kwenye mpango wa kubadilisha wahamiaji

Australia na Malaysia kwenye mpango wa kubadilisha wahamiaji

Umoja wa Mataifa hii leo umesisitiza umuhimu wa kuhakikisha kuwa usalama umedumishwa wakati wa kutekelezwa kwa mpango wa kubadilisha watafuta hifadhi kati ya mataifa ya Australia na Malaysia kama moja ya njia ya kukabiliana na kusafirishwa kwa watu kiharamu na safari hatari ambazo husababisha kupotea kwa maisha.

Kwenye makubaliano hayo yaliyotiwa sahihi hii leo kati ya serikali zote mbili , Australia itatuma watafuta hifadhi 800 kwenda Malaysia kwa muda wa miaka minne ijayo ili kubadilishana na watafuta hifadhi 4000 wanaotafuta hifadhi nchini Australia ambao kwa sasa wako nchini Malysia. Shirika la kuhudumia wakimbizi la moja wa Mataifa UNHCR linasema kuwa lina matumani kuwa mpango huo utaleta usalama baina ya nchi hizo mbili na eneo zima.