Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Bi. Amos aelezea wasiwasi uliopo kwa kupungua kwa misaada kwenye eneo la Kordofan Kusini

Bi. Amos aelezea wasiwasi uliopo kwa kupungua kwa misaada kwenye eneo la Kordofan Kusini

Mratibu wa masuala ya kibinadamu kwenye Umoja wa Matifa Valerie Amos ameelezea wasi wasi uliopo wakati kunapoendelea kushuhudiwa upungufu wa misaada kwa watu waliojipata kwenye mapigano ya hivi majuzi kwenye eneo la Kordofan Kusini nchini Sudan akionya kuwa huenda hali hiyo ikasababisha madhara zaidi.

Maelfu ya watu wamelazimika kuhama makwao huku idadi ya wengine isiyojulikana wakiuawa tangu kuanza kwa mapigano hayo mapema mwezi Juni kati ya wanajeshi wa serikali ya Sudan na kundi la kaskazini la Sudan People's Liberation Movement (SPLM-N) lililopigana vita vya muda mrefu vilivyomalizika mwaka 2005.

Hata hivyo Amos amesema kuwa washirika wa kutoka huduma za kibinadam waliokuwa kwenye eneo hilo kabla ya kuanza kwa mzozo wamesambaza misaada ya dharura ikiwemo vyakula na madawa kwa zaidi ya watu 70,000 kwenye sehemu za milima za Kordofan Kusini. Amos pia ametoa wito kwa pande husika kuruhusu kupelekwa kwa misaada akiongeza kuwa ikiwa watazuia itakuwa vigumu kuwahudumia raia wanaohitaji usaidizi.