Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Huenda hali iliyopo kwenye pembe ya Afrika ikawa janga la kibinadamu

Huenda hali iliyopo kwenye pembe ya Afrika ikawa janga la kibinadamu

Huenda hali mbaya ya ukame kwenye pembe ya Afrika  ikabadilika na kuwa janga la kibinadamu ambalo litaathiri eno kubwa. Hii ni kulingana na mkutano wa dharura wa mawaziri wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mashirika yasiyokuwa ya kiserikali uliofanyika mjini Rome kulijadili janga hilo linalozidi kuongezeka.

Mkutano huo ulioandaliwa na shirika la kilimo na mazao la Umoja wa Matifa FAO unasema kuwa ni suala muhimu kuwa mahitaji ya watu wanaoathiriwa na ukame yanashughulikiwa sasa. Uhaba wa chakula kwenye pembe ya Afrika uliosababishwa na ukame ambao hujashuhudiwa kwa kipindi cha miaka 60 iliyopita unawaathiri watu milioni 12. Josette Sheeran, ni mkurugenzi wa FAO.

( SAUTI YA JOSETTE SHEERAN)