Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uhaba mkubwa wa chakula waendelea kushuhudiwa kwenye Pembe ya Afrika

Uhaba mkubwa wa chakula waendelea kushuhudiwa kwenye Pembe ya Afrika

Makala yetu ya wiki hii inaangazia hali kwenye pembe ya Afrika eneo ambalo limekumbwa na ukame wa muda mrefu na kusababisha uhaba mkubwa wa chakula.

Zaidi ya watu milioni moja wanahitaji misaada ya kuokoa maisha wakati kunaposhuhudiwa hali mbaya zaidi ya ukame ambayo haijawai kushudiwa kwa miongo kadha kwenye nchi za pembe ya Afrika.

Nchi za pembe ya Afrika zikiwemo Somalia, Kenya , Djibouti na Ethiopia pamoja na mataifa mengine ya eneo la kaskazini mashariki mwa Afrika zinaendelea kukumbwa na uhaba mkubwa wa chakula hali iliyotajwa na mkuu wa shirika la kuwahudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR Antonio Guterres kama janga mbaya zaidi la kibinadamu duniani baada ya kulitembelea eneo hilo hivi majuzi.