Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Msaada wa kufadhili uvumbuzi wa matumizi ya taka za binadamu watolewa

Msaada wa kufadhili uvumbuzi wa matumizi ya taka za binadamu watolewa

Mjumbe wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki ya kuwa na maji na usafi wa mazingira amekaribisha msaada ya mailioni ya dola ulitolewa na wakfu wa Bill na Melinda Gates utakaotumika kuboresha choo kwa lengo la kubadili taka za binadamu ili kutumika kwa kuzalisha kawi na mbolea. Catarina de Albuquerque hata hivyo ameonya kuwa itahitaji uvumbuzi zaidi kuweza kukabiliana na tatizo la usafi wa mazingira duniani.

Amesema kuwa kutoa hamasisho kuhusu umuhimu wa usafi wa mazingira ni suala muhimu . Mapema juma hili wakfu huo ulitangaza msaada wa dola milioni 42 ili kufadhili uvumbuzi kuhusu njia zinazoweza kutumika kubadilisha taka za binadamu kutumika kuzalisha kawi, kama mbolea au kama maji.