Skip to main content

Tume ya Cameroon na Nigeria yakutana kutatua mzozo wa mpaka

Tume ya Cameroon na Nigeria yakutana kutatua mzozo wa mpaka

Tume ya pamoja ya Cameroon na Nigeria inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa imeanza mkutano wao hii leo mjini Abuja Nigeria ili kuendelea na mzungumzo kuhusu masuala yaliyosalia ya mpaka kati ya matiafa hayo mawili jirani. Tume hii iliyobuniwa na Umoja wa Matifa kwa ombi la Cameroon na Nigeria ili kutekeleza uamuzi wa mahakama ya haki ya kimataifa ICJ wa kuchorwa kwa mpaka imefikia uamuzi wa kilomita 1600 kati ya kilomita zote 1950.

Ofisi ya Umoja wa Mataifa katika eneo la Afrika Magharibi inasema kuwa tume hiyo itaangazia hatua zinazostahili kuchukuliwa ili kuyafanya makubaliano hayo kuwa vitendo. Tume hiyo inawajumuisha wajumbe kutoka Cameroon , Nigeria na Umoja wa Mataifa na kuongozwa na mjumbe maalum wa Matibu mkuu wa Umoja wa Mataifa katika eneo la Afrika Magharibi Saïd Djinnit.