Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ufadhili mpya uliobuniwa wa kusaidia kuhifadhi familia za mifugo wapokea msaada

Ufadhili mpya uliobuniwa wa kusaidia kuhifadhi familia za mifugo wapokea msaada

Ufadhili mpya uliobuniwa kwa lengo la kuzisadia nchi zinazoendelea kuhifadhi familia na kutumia mifugo wao kwa njia inayofaa umepokea msaada wake wa kwanza wa jumla la dola milioni 100 kutoka Ujerumani, Norway na Uswisi. Fedha hizo zitagharamia miradi inayotolewa na serikali kulingana na mipango ya kimataifa ya uhifadhi wa genetiki za wanyama.

Asilimia 21 ya familia 8000 ya mifugo duniani imetajwa kuwa kwenye hatari ya kuangamia. Tangu kutangazwa kwa mpango huo nchi zinazoripoti kuhusu idadi ya familia za mifugo imeongezeka ishara kuwa kupotea kwa mifugo kumepungua.