Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Janga la njaa nchini Somalia ni athari kubwa kwa watoto:UNICEF

Janga la njaa nchini Somalia ni athari kubwa kwa watoto:UNICEF

Watoto ndio wametajwa kuathirika zaidi na hali ya njaa ambayo imetangazwa katika maeneo mawili ya kusini mwa Somalia ya Bakool Kusini na Lower Shabelle. Shirika la kuwahudumia watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF linasema kuwa mmoja kati ya watoto watatu kwenye maeneo yaliyoathirika anasumbuliwa na ukame na sita kati ya watoto 10,000 walio chini ya miaka mitano wanakufa kila siku.UNICEF inasema kuwa watoto nusu milioni wako kwenye hatari ya kupoteza maisha yao.

(SAUTI YA ALICE KARIUKI)