Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM waendelea na juhudi za utoaji misaada nchini Somalia

UM waendelea na juhudi za utoaji misaada nchini Somalia

Umoja wa Mataifa unaendelea na juhudi zake za kuwalisha mamilioni ya watu nchini Somalia ambapo njaa imetangazwa kwenye maeneo mawili nchini humo. Shirika la mpango wa chakula dunia WFP linasema kuwa watu milioni 11.3 wanahitaji chakula. Pembe ya Afrika inakabiliwa na ukame ambalo hujawai kushuhudiwa katika eneo hilo kwa miaka mingi iliyopita hali ambayo imewalazimu watu kukimbia makwao wakitafuta chakula na maji.

Mkuruegenzi mku wa WFP Josette Sheeran yuko nchini Somalia na huenda akalitembelea eneo lote hilo siku zinazokuja. Siku ya Jumatatu shirika la kilimo na mazao la Umoja wa Mataifa FAO litaandaa mkutano wa kukusanya misaada ili kuweza kukabiliana na hali hiyo.